About
The Swahili Colloquium has become a well-established forum in Bayreuth. Founded in 1987, the Colloquium has regularly been supported by the German Research Council (DFG). Every year, we invite scholars and researchers from different disciplines, who work on various aspects of the language and the respective culture(s) of Eastern Africa and the diaspora. The multidisciplinary approach and the wide range of contributions from Linguistics and Literary Studies to Anthropology and History particularly account for its appeal. We are always looking forward to welcoming new participants at the Swahili Colloquium. The conference languages are Swahili and English.
Kongamano hili la kila mwaka la Kiswahili limeshaota mizizi hapa katika Chuo Kikuu cha Bayreuth. Lilianzishwa mwaka wa 1987. Kila baada ya miaka miwili limefadhiliwa na Shirika la Utafiti la Kijerumani (DFG). Mwaka baada ya mwaka kongamano linawakaribisha wataalamu wa masomo mbalimbali wanaojishughulisha na uchunguzi wa vipengele kadha wa kadha vinavyohusu Kiswahili na tamaduni zake. Upana wa mada zinazohusu Kiswahili na zinazozungumziwa kwenye Kongamano ni pana sana; nazo mada hizi ni kuanzia isimu, masomo ya fasihi mpaka anthropolojia, historia na jiografia, kwa kutaja chache tu, jambo ambalo linalipa kongamano hili msingi wa nguvu. Katika fursa hii wataalamu wanaojishughulisha na masomo anuwai kutoka pembe mbalimbali za dunia hupata kubadilishana mawazo. Wasanii, wahakiki na mashabiki wa fani mbalimbali za Kiswahili pia hujiunga nasi. Bali na furaha tuliyo nayo kuwakaribisha wale ambao wamezoea kuja hapa Bayreuth miaka iliyopita, tunafurahi kuwapokea na kuwakaribisha wataalamu, wanafunzi na mashabiki wapya, na wala yeyote asisite kupanga kuja. Lugha za mawasiliano ni Kiswahili na Kiingereza.