Team >
Gerlind Scheckenbach (4.10.1948 -12.7.2021)
Leo tumepata habari ya kusikitisha kwamba mwalimu wetu wa Kiswahili wa zamani, Gerlind Scheckenbach, aliaga dunia hii ambayo si yetu. Gerlind Scheckenbach alinifundishia mimi maneno yangu ya kwanza ya Kiswahili – kama alivyowafundishia wanafunzi wengi wa chuo kikuu chetu cha Bayreuth kabla ya kustaafu mwaka wa 2013. Kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Bayreuth katika miaka tisini, Gerlind alikuwa ameishi kusini ya Tanzania pamoja na familia yake kwa miaka minane. Tanzania alichangia katika miradi mbalimbali ya kuwasaidia na kuwafundisha watoto walemavu. Alikuwa amefanya masomo ya psychologia na alikuwa tayari anafanya kazi katika taasisi na shule za walemavu Ujerumani. Alikuwa ni mtu ambaye alipenda kuwasaidia watu. Na hata wakati wa kufundisha Kiswahili chuoni, alikuwa mwalimu wa kipekee, kwa sababu hakuwa mwalimu hodari wa kufundisha tu, lakini vilevile aliwakaribisha wanafunzi wote kwa mikono miwili na moyo mkunjufu. Alitufundishia kupenda lugha ya Kiswahili, misemo yake na fasihi yake, na vilevile, kwa wale wanafunzi ambao walikuwa wazito wa kuelewa, aliwaalika kwa masomo ya ziada nyumbani ili kuhakikisha kila mwanafunzi afaulu mtihani. Pia hakuchoka kuwasikiliza wale ambao walikuwa na shida nyumbani ama walikuwa hawana pesa ama wale ambao walikuwa na wasiwasi nyingi kwa sababu ya masomo. Alitufundishia mengi na aliwatia wote moyo. Roho nyingi zimepona kwake.
Mwalimu wetu hakujiweka kwenye mstaari wa mbele kwa upande wa utafiti, alikuwa mpole na mkimya, lakini alichangia katika maandishi na miradi mingi ya idara kama utafiti kuhusu mashairi ya Fumo Liyongo ama baadaye mashairi ya Zahidi Mngumi. Pia, alitoa msaada wakati wa scanning ya kamusi ya Sacleux. Kwa upande wa utafiti wake binafsi, alichunguza msamiati na maneno ambayo yanarejelea walemavu na ulemavu katika lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu kwa jumla. Pamoja na mwalimu Thilo Schadeberg na mwalimu Abel Mreta, aliandika makala nzuri kuhusu ngeli za kibantu na maneno yanayorejelea walemavu (Mreta, Abel Y., Thilo C. Schadeberg & Gerlind Scheckenbach. 1997. 'Kiziwi, Kipofu na Kilema: Ubaguzi au Heshima?'. In: Rose-Marie Beck, Thomas Geider, Werner Graebner & Ingo Heine (eds), Swahili Forum IV. (Afrikanistische Arbeitspapiere, No. 51). Köln: Institut für Afrikanistik, Universität Köln. Pp. 23-54).
Pia ninapenda sana mchango wake (kwa Kijerumani) kuhusu maana ya busara (Scheckenbach, G. 2006. ‘Busara: Besonnenheit und Takt.’ In: K. Winkelmann & D. Ibriszimow (eds). Zwischen Bantu und Burkina. Festschrift für Gudrun Miehe. Cologne: Köppe. Pp. 207-234). Katika makala hiyo anatofautisha busara na hekima na akili kwa upande wa maana zao za asili katika lugha za kisemitiki na pia kwa matumizi ya siku hizi, na anaonyesha kwamba busara ina kipengele ya kuwatenda watu wengine vema (tofauti na hekima na akili). Mwenye busara ni mtu ambaye anamjali mwenzake, anamonyesha heshima na anayemwelewa bila ya maneno mengi. Katika makala yake, anamdondoa shairi la Shaaban Robert la busara. Katika shairi hilo, busara ni mtu na anasema: “palipo matengenezo nikiwapo mimi ndani.” (Robert, Sanaa ya Ushairi, 10f.). Sisiti kumwita Gerlind mwenye busara. Mngu amlaze mahali pema.
- Clarissa Vierke
Gestern bekamen wir die traurige Nachricht, dass Gerlind Scheckenbach (4.10.1948-12.7.2021) gestorben ist. Gerlind Scheckenbach war bis zu ihrem Ruhestand 2013 Swahili-Lektorin und hat mir und vielen anderen Studierenden an der Universität Bayreuth die ersten Worte Swahili beigebracht und die Liebe zu dieser ostafrikanischen Sprache vermittelt. Die Diplompsychologin kam in den 1990er Jahren an die Uni Bayreuth. Vorher hatte sie mit ihrer Familie acht Jahre im Süden Tansanias gelebt, wo sie sich in vielen Projekten und Institutionen für Kinder mit Behinderungen engagierte. Schon vorher Deutschland hatte sie in der Lebenshilfe mit und für Kinder mit Behinderungen gearbeitet.
An der Universität Bayreuth war sie eine unermüdlich engagierte Lektorin, die mit viel Ausdauer, didaktischem Geschick und Verständnis den Studierenden Swahili beibrachte. Darüber hinaus hatte sie immer für Studierende Zeit, gab Extrastunden Nachhilfe für die, denen die fremde Struktur der Sprache schwerfiel. Aber auch für anderen Sorgen der Studierenden - sei es in der Familie, Geldsorgen oder Ängste wegen des Studiums - hatte sie immer ein offenes Ohr. Sie ermutigte, korrigierte in ihrer Freizeit unzählige afrikanistische Abschlussarbeiten und hatte immer einen Tee bereit für alle, die vorbeikamen.
Mit ihrer intelligenten, stillen und überlegten aber humorvollen Art brachte sie sich in die verschiedenen Studiengängen der Afrikanistik ebenfalls stetig ein, betreute Gäste und arbeitete auch an der Forschung in der Afrikanistik, etwa zur Epen-Dichtung des 18. Jahrhunderts, aktiv mit. In ihrer eigenen Forschung beschäftigte sie sich vor allem vergleichend mit Termini für Behinderungen und Behinderte im Swahili und anderen Bantusprachen.
Wir alle aus der Bayreuther Afrikanistik betrauern den Tod einer herausragenden Lehrerin, tollen Kollegin und lieben Freundin! Mungu amlaze mahali pema.
- Clarissa Vierke